Home » Orodha ya Walioitwa kwenye usaili Manispaa ya Temeke 2026
Interview

Orodha ya Walioitwa kwenye usaili Manispaa ya Temeke 2026

Hii hapa orodha ya majina ya walioitwa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imetangaza usaili wa ajira za kada za afya kuanzia tarehe 01 Juni hadi 05 Juni 2026. Soma ratiba na maelekezo muhimu kwa wasailiwa hapa.

Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Temeke Manispaa

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke amewataarifu waombaji wa nafasi mbalimbali za kazi katika kada ya afya zilizotangazwa tarehe 09/03/2026 kuwa usaili unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 01 Juni 2026 hadi 05 Juni 2026.

Pakua PDF ya majina hapa

Usaili huo utafanyika katika ukumbi wa Idd Nyundo uliopo Manispaa ya Temeke.

Tarehe za Usaili Temeke 2026

Ratiba ya Usaili

  • Kuanzia: 01/06/2026
  • Hadi: 05/06/2026

Muda wa Usaili

  • Kuanzia saa 1:00 Asubuhi

Ratiba ya tarehe kwa kila kada imeainishwa kwenye orodha rasmi ya waombaji walioitwa kwenye usaili.

Eneo la Kufanyia Usaili

Usaili wote utafanyika katika:

Ukumbi wa Idd Nyundo

  • Manispaa ya Temeke
  • Dar es Salaam

Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa

Waombaji wote wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:

1. Kitambulisho kwa Ajili ya Utambuzi

Kila msailiwa anatakiwa kuwa na kitambulisho halali. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:

  • Kitambulisho cha Mkazi
  • Kitambulisho cha Mpiga Kura
  • Kitambulisho cha Kazi
  • Kitambulisho cha Uraia
  • Hati ya Kusafiria
  • Leseni ya Udereva
  • Barua ya Utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa au Kijiji

Vyeti Vinavyotakiwa Kwenye Usaili

Wasailiwa wanapaswa kufika na vyeti halisi vya:

  • Cheti cha Kuzaliwa
  • Kidato cha IV
  • Kidato cha VI
  • Astashahada
  • Stashahada
  • Shahada

Kada Zinazohitaji Leseni na Usajili

Kwa kada zinazohitaji leseni na usajili wa kitaaluma, waombaji wanapaswa kuwasilisha:

  • Leseni halali
  • Vyeti vya usajili wa Baraza husika la kitaaluma

Nyaraka Zisizokubalika

Waombaji watakaowasilisha nyaraka zifuatazo hawataruhusiwa kuendelea na usaili:

  • Testimonials
  • Provisional Results
  • Statement of Results
  • Form IV Results Slips
  • Form VI Results Slips

Gharama za Wasailiwa

Kila msailiwa atajigharamia:

  • Chakula
  • Usafiri
  • Malazi

Tofauti za Majina Kwenye Vyeti

Waombaji wenye tofauti za majina kwenye:

  • Cheti cha kuzaliwa
  • NIDA
  • Vyeti vya taaluma

Wanapaswa kuwa na:

Deed Poll

Kutoka kwa Kamishina wa Ardhi.

Kwa wale wenye tofauti za herufi pekee kwenye majina, wanatakiwa kuwasilisha:

Affidavit (Kiapo cha Majina)

Hitimisho

Waombaji wote walioitwa kwenye usaili wa Temeke Municipal Council wanashauriwa kufika kwa wakati, kujiandaa vizuri, na kuhakikisha wanazingatia maelekezo yote yaliyotolewa kwenye tangazo rasmi la usaili ili kuepuka usumbufu siku ya usaili.

Soma zaidi: Tangazo la Usaili NIMR, TAWA 2026