Hii hapa orodha ya majina ya walioitwa kwenye inteview Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ametangaza ratiba ya usaili wa ajira kwa waombaji kazi walioitwa kwenye usaili utakaofanyika kuanzia tarehe 19 Juni 2026 hadi 20 Juni 2026. Waombaji waliochaguliwa wanatakiwa kuhudhuria usaili katika muda na eneo lililotajwa kwa kada husika, wakiwa na kitambulisho halali pamoja na vyeti vyao halisi vya elimu kuanzia cheti cha kuzaliwa, Kidato cha Nne, Kidato cha Sita, Astashahada, Stashahada, Shahada na vyeti vingine vinavyotakiwa. Majina ya walioitwa kwenye usaili wa Pangani 2026 yanaweza kuangaliwa kupitia mfumo wa Ajira Portal ambapo wasailiwa wanapaswa pia kunakili namba zao za usaili kabla ya siku ya usaili.
Halmashauri ya Wilaya ya Pangani imeeleza kuwa nyaraka kama Testimonials, Provisional Results, Statement of Results na Result Slips za Form Four au Form Six hazitakubaliwa katika usaili. Aidha, waombaji waliosoma nje ya Tanzania wanapaswa kuwasilisha vyeti vilivyohakikiwa na TCU, NACTVET au NECTA kulingana na ngazi ya elimu. Waombaji wote wanakumbushwa kuwa mchakato wa ajira unazingatia haki, usawa na uwazi, huku vitendo vya rushwa vikikatazwa kabisa. Waombaji ambao hawakuona majina yao kwenye orodha ya walioitwa wanashauriwa kuingia kwenye akaunti zao za Ajira Portal ili kuona sababu za kutokuitwa kwenye usaili na kujipanga kwa fursa zijazo.
Usaili wa Ajira Halmashauri ya Wilaya ya Pangani 2026 utafanyika tarehe 19 hadi 20 Juni 2026. Angalia majina ya walioitwa kwenye usaili, maelekezo muhimu na nyaraka zinazohitajika.
Soma zaidi: Tangazo la Sekretarieti ya Ajira
Add Comment