Hii hapa Orodha ya Majina ya walioitwa kwenye Usaili Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida ametangaza rasmi ratiba ya usaili wa ajira kwa waombaji kazi walioitwa kwenye usaili utakaofanyika kuanzia tarehe 23 Juni 2026 hadi 26 Juni 2026. Wasailiwa wanatakiwa kufika katika eneo la usaili kwa muda uliopangwa, wakiwa na kitambulisho halali cha utambuzi pamoja na vyeti halisi vya elimu kuanzia cheti cha kuzaliwa, Kidato cha Nne, Kidato cha Sita, Astashahada, Stashahada, Shahada na vyeti vingine vinavyohitajika kwa kada husika. Majina ya walioitwa kwenye usaili wa Manispaa ya Singida 2026 yanapatikana kupitia mfumo wa Ajira Portal ambapo kila mwombaji anatakiwa kunakili namba yake ya usaili kabla ya tarehe ya usaili.
Waombaji wote wanakumbushwa kuwa testimonials, provisional results, statement of results pamoja na result slips za Form Four na Form Six hazitakubaliwa wakati wa usaili. Aidha, waombaji waliosoma nje ya Tanzania wanapaswa kuhakikisha vyeti vyao vimehakikiwa na mamlaka husika kama NECTA, TCU au NACTVET. Halmashauri ya Manispaa ya Singida imesisitiza kuwa mchakato wa ajira unazingatia haki, usawa na uwazi, huku ikikataza vitendo vyote vya rushwa katika kupata ajira au kupangiwa vituo vya kazi. Waombaji ambao hawakuona majina yao wanashauriwa kuingia kwenye akaunti zao za Ajira Portal ili kuona sababu za kutoitwa kwenye usaili.
Usaili wa Ajira Manispaa ya Singida 2026 utafanyika kuanzia tarehe 23 hadi 26 Juni 2026. Angalia maelekezo ya usaili, nyaraka zinazohitajika, na majina ya walioitwa kwenye usaili kupitia Ajira Portal.
Soma zaidi: Tangazo la Sekretarieti ya Ajira
Add Comment