Hii hapa orodha ya majina ya walioitwa kwenye interview Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe ametangaza rasmi ratiba ya usaili wa ajira kwa waombaji kazi walioomba nafasi mbalimbali, ambapo usaili utafanyika kuanzia tarehe 19 Juni 2026 hadi 26 Juni 2026. Waombaji walioitwa kwenye usaili wa Korogwe 2026 wanatakiwa kufika katika eneo na muda uliopangwa kwa kada husika wakiwa na kitambulisho halali pamoja na vyeti vyao halisi vya elimu kuanzia cheti cha kuzaliwa, Kidato cha Nne, Kidato cha Sita, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu na Shahada kulingana na sifa za nafasi waliyoomba. Wasailiwa wote wanapaswa kuingia kwenye mfumo wa Ajira Portal ili kunakili namba zao za usaili kabla ya siku ya usaili.
Halmashauri ya Mji wa Korogwe imeeleza kuwa nyaraka kama Testimonials, Provisional Results, Statement of Results pamoja na Form IV na Form VI Result Slips hazitakubaliwa wakati wa usaili. Aidha, waombaji waliosoma nje ya Tanzania wanapaswa kuhakikisha vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika kama TCU, NACTVET au NECTA. Waombaji wote wanakumbushwa kuwa mchakato wa ajira unazingatia misingi ya haki, usawa na uwazi, huku vitendo vya rushwa vikikatazwa kabisa katika hatua zote za ajira na upangaji wa vituo vya kazi. Waombaji ambao hawakuona majina yao kwenye orodha ya walioitwa wanashauriwa kuangalia sababu za kutokuitwa kupitia akaunti zao za Ajira Portal.
Usaili wa Ajira Halmashauri ya Mji wa Korogwe 2026 utafanyika kuanzia tarehe 19 hadi 26 Juni 2026. Angalia majina ya walioitwa kwenye usaili, maelekezo muhimu na nyaraka zinazohitajika.
Soma zaidi: Tangazo la Sekretarieti ya Ajira
Add Comment