Home » Orodha ya Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Wilaya ya Igunga 2026
Interview

Orodha ya Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Wilaya ya Igunga 2026

Hii hapa orodha ya majina ya walioitwa kwenye interview Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ametangaza rasmi usaili wa ajira kwa waombaji kazi walioomba nafasi mbalimbali, ambapo usaili utafanyika kuanzia tarehe 23 Juni 2026 hadi 24 Juni 2026. Waombaji walioitwa kwenye usaili wa Igunga 2026 wanatakiwa kuhudhuria katika muda na eneo lililotajwa kwa kada husika wakiwa na kitambulisho halali pamoja na vyeti vyao halisi vya elimu kuanzia cheti cha kuzaliwa, Kidato cha Nne, Kidato cha Sita, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu na Shahada kulingana na sifa za nafasi waliyoomba. Wasailiwa wote wanapaswa pia kuingia kwenye akaunti zao za Ajira Portal ili kunakili namba za usaili kabla ya tarehe ya usaili.

Halmashauri ya Wilaya ya Igunga imeeleza kuwa nyaraka kama Testimonials, Provisional Results, Statement of Results na Form IV au Form VI Result Slips hazitakubaliwa wakati wa usaili. Aidha, waombaji waliosoma nje ya Tanzania wanapaswa kuwasilisha vyeti vilivyohakikiwa na TCU, NACTVET au NECTA pamoja na cheti cha GPA kwa kada zinazohitaji ukokotozi huo. Mchakato wa ajira unazingatia misingi ya haki, usawa na uwazi, huku waombaji wakikumbushwa kuwa ni marufuku kutoa au kupokea rushwa kwa lengo la kupata ajira au kupangiwa kituo cha kazi. Waombaji ambao hawakuona majina yao wanashauriwa kuangalia sababu za kutokuitwa kupitia akaunti zao za Ajira Portal.

Usaili wa Ajira Halmashauri ya Wilaya ya Igunga 2026 utafanyika tarehe 23 hadi 24 Juni 2026. Angalia majina ya walioitwa kwenye usaili, maelekezo muhimu na nyaraka zinazohitajika.

Soma zaidi: Tangazo la Sekretarieti ya Ajira